Staa wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe amerejea katika mazoezi ndani ya klabu yake siku chache baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia.

Katika hali ambayo sio ya kawaida kwa mchezaji huyo kurejea mazoezini mapema, Kwani staa huyo alicheza fainali ya kombe la dunia siku ya jumapili ambapo walipoteza kwa mikwaju ya penati dhidi ya timu ya taifa ya Argentina.mbappeKitendo alichokifanya Mbappe kimefanya watu wengi kumpongeza, Kwani hii inatokea mara chache kwa mchezaji mwenye hadhi kama yake kuwahi mazoezini mapema ikizingatiwa ametoka kucheza mchezo wa fainali katika siku tatu zilizopita.

Mchezaji huyo amerejea katika kambi ya klabu hiyo siku moja baada ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa ambapo mchezaji huyo amefanikiwa kutimiza umri wa miaka 24, Na leo amefika katika viwanja vya mazoezi vya klabu hiyo.mbappeMchezaji Kylian Mbappe ameonekana kufata nyendo za staa ambae anamtazama kama kioo chake Cristiano Ronaldo ambae amekua akisifika zaidi kua mchezaji mwenye nidhamu ya mazoezi kwa kiwango kikubwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa