Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amesema beki wake raia wa Argentina Lisandro Martinez alitaka kuja kwenye klabu hiyo wakati anataka kuondoka klabu ya Ajax.

Beki huyo ambaye ametwa ubingwa wa kombe la dunia timu ya taifa ya Argentina wikiendi iliyomalizika, Lisandro Martinez alipanga kuondoka kwenye klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi katika dirisha la usajili lililomalizika.ten hagKocha Erik Ten Hag anasema beki huyo alimpigia simu wakati anataka kuondoka katika klabu ya Ajax na kumueleza kua anataka kuondoka klabuni hapo na ataelekea klabu ya Arsenal ambayo ilituma ofa nzuri klabuni hapo, Lakini beki huyo akamuambia kocha huyo kama anahitaji huduma yake yupo tayari kuungana nae.

Beki Lisandro Martinez alikua chini ya kocha Erik Ten Hag ndani ya kjlabu ya Ajax kabla ya kuundoka klabuni hapo na kujiunga na mashetani wekundu, Hivo beki huyo alipoonesha nia ya kuungana na mwalimu wke huyo kocha huyo hakua na pingamizi juu ya uamuzi huo.ten hagBeki Lisandro Martinez amekua kwenye ubora mkubwa tangu ajiunge katika klabu ya Manchester United na kufanikiwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo, Huku akitengeneza ushirikiano mzuri na beki wa kimataifa wa Ufaransa Raphael Varane.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa