Kiungo wa zamani wa klabu ya Azam Fc Ibrahim Ajibu Migomba ameagwa rasmi na iliyokua klabu yake klabu ya Azam Fc ikielezwa anatimkia klabu ya Singida Big Stars.

Mchezaji huyo inaelezwa yupo kwenye hatua za mwisho za kujiunga na klabu ya Singida Big Stars ya mkoani Singida baada ya kuhudumu kwa waoka mikate wa Azam kwa takribani mwaka mmoja na nusu.ibrahimu ajibuNyota Ibrahim Ajibu wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga amekua hayupo kwenye kiwango bora sana tangu alipoondoka ndani ya klabu ya Yanga, Hivo kumfanya kutopata nafasi katika vilabu vya Azam na Simba huku kwasasa akiwa anasubiriwa ndani ya klabu ya Singida Bid Stars.

Klabu ya Singida Big Stars imeonekana miongoni mwa vilabu tishio katika ligi kuu ya NBC msimu huu kutokana na sajili ambazi wamekua wakizifanya, Mpaka sasa klabu hiyo imeshafanya sajili za wachezaji kama Nickson Kibabage na Ibrahim Ajib ambaye yupo hatua za mwishoni kujiunga klabuni hapo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa