Kiungo wa zamani wa klabu ya Real Madrid Isco Alarcon amevunja mkataba na mkataba na klabu yake ya Sevilla ambayo alikua anaitumikia tangu mwezi Agosti mwaka huu.

Nyota huyo ambaye alijiunga na klabu ya Sevilla mwaka huu mwezi wa nane akitokea klabu ya Real Madrid, Ameamua kuvunja mkataba na klabu ya Sevilla kwa makubaliano ya pande zote mbili hivo mchezaji huyo yupo huru kujiunga na klabu yeyote.iscoKiungo Isco Alarcon ambaye amepata mafanikio makubwa na klabu ya Real Madrid akiwa kwenye rekodi ya wachezaji wachache waliobeba mataji matano ya ligi ya mabingwa ulaya na klabu ya Real Madrid.

Kiungo huyo fundi ambaye alikua mchezaji muhimu wa klabu ya Sevilla tangu amejiunga klabuni hapo akifanikiwa kuanza michezo 16 kati ya 19 aliyocheza klabuni hapo, Huku pia akifanikiwa kuhusika kwenye mabao  manne ya klabu hiyo huku akifunga moja na kutengeneza matatu.iscoKiungo Isco baada ya kuachana na klabu ya Sevilla amekua akihusishwa na vilabu vya Napoli, Juventus, Aston Vila Huku pia akihusishwa na kocha wake wa zamani ndani ya klabu ya Real Madrid ambaye amejiunga na klabu ya Wolves Julien Lopetegui.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa