Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amesema wakishinda taji la ligi kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga itaonesha wameanza kurejesha ubora wao.

Klabu ya Fc Barcelona imekua ikipitia kipindi kigumu kwenye suala la kiuchumi na matokeo mabaya kiwanjani kwa miaka ya karibuni ambayo imekua ikiiweka klabu hiyo kwenye wakati mgumu sana.laportaKlabu ya Fc Barcelona imeshinda taji la La liga mara ya mwisho ilikua mwaka 2018/19 huku wakitolewa mara mbili kwenye hatua ya makundi kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya taji ambalo wameshinda mwaka 2015.

Rais Laporta anasema kua lengo kubwa msimu huu ni kushinda taji la La liga na kuongeza kua wakifanikiwa kushinda taji hilo itaonesha taratibu wanarejea kwenye ubora wao ambao wameupoteza kwa muda mrefu.laportaRais Joan Laporta anataka kuhakikisha anairudisha klabu ya Bracelona kwenye zama zake baada ya kuichukua klabu hiyo chini ya rais aliepita Josep Maria Bartomeu, Hii ni mara ya pili kwa Laporta kuiongoza klabu hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa