Blatter Amshutumu Infantino

Rais wa zamani wa shirikisho la soka duniani (FIFA) Sepp Blatter amesema Rais wasasa wa shirikisho hilo Gianni Infantino baada ya kuongeza timu kwenye michuano ya kombe la dunia kutoka 32 mpaka 48.

Rais wa Infantino amefanya mabadiliko kwenye michuano ya kombe la dunia kuanzia ngazi ya taifa na vilabu kutoka timu 32 kwenye ngazi ya taifa mpaka 48 na ngazi ya klabu bingwa ya dunia kutoka timu sita mpaka 35.blatterRais wa zamani Blatter yeye anaona kama tamaa ya biashara ambayo Infantino anataka kuingiza kwenye mpira wa miguu baada ya kuongeza timu kwenye michuano ya kombe la dunia ya klabu na timu za taifa.

Rais wa zamani wa shirikisho hilo pia ameendelea kumshutumu mrithi wake Infantino na kusema hawana mahusiano mazuri na Rais huyo kwakua amegoma kuzungumza nae tangu amechaguliwa kua Rais wa shirikisho hilo.blatterRais huyo wa zamani wa shirikisho hilo bwana Sepp Blatter amesema anachokifanya Gianni Infantino kuongeza timu kwenye michuano hiyo ni kutaka kushindana na ligi ya mabingwa ulaya, Ambapo kimsingi anaamini ni kazi ambayo haiwahusu.

 

Acha ujumbe