Kocha wa klabu ya Manchester United Pep Guardiola amepigilia msumari kua nyota wa klabu ya PSG na timu a taifa ya Argentina Lionel Messi kua ndio mchezaji bora duniani kuwahi kutokea.

Lionel Messi ambaye amekua akitajwa kama mchezaji bora kuwahi kutokea lakini watu wengi bado walikua wanamuekea mashaka kumuweka kwenye sentensi moja na magwiji kama Pele na Maradona, Lakini siku ya jumapili alifanikiwa kukata mzizi wa fitina baada ya kutwaa kombe la dunia.guardiolaKocha wa Manchester City Guardiola ambaye amewahi kumfundisha Messi katika klabu ya Barcelona, Yeye amesema kua nyota huyo ndio mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea na wanaosema kua ni Pele au Maradona wanaongea kwa hisia.

“Kila mtu ana maoni yake, Lakini hakuna anayeweza kutilia shaka kua yeye ni Bora zaidi wa wakati wote, Kwangu nimesema mara nyingi kua yeye ndio bora zaidi. Watu waliofanikiwa kumuona Pele, Alfredo di Stefano, Maradona wanaweza kusema huyu ndio kipenzi changu lakini maoni haya ni ya hisia”guardiolaKocha Pep Guardiola amesema yeye kwake ni mchezaji bora wa muda wote, Licha ya maneno mengi ya kua hakua amebeba kombe la dunia, Lakini kwa kocha huyo amesema hata Messi asingebeba kombe la dunia kwake yeye kisingebadilika kitu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa