Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amefanikiwa kuongeza mkataba na klabu hiyo utakaomweka klabuni hapo mpaka 2025.

Kocha huyo raia wa Hispania ambaye amejiunga klabuni hapo mwezi Juni 2016 amefanikiwa kuifanya timu hiyo kua bora na tishio kunako ligi ya Uingereza pamoja na barani ulaya kwa ujumla. Kocha huyo anasifika zaidi kwa soka lake la kuvutia pamoja kumiliki mpira kwa muda mrefu amemwaga wino kusalia klabuni hapo mpaka 2025.GuardiolaPep Guardiola amekua kocha wa kwanza kuipa klabu hiyo mataji manne ya ligi kuu ya Uingereza kwa kipindi cha miaka sita klabuni hapo jambo linalomfanya kua kocha aliefanikiwa zaidi kwenye historia ya klabu ya Manchester City.

Kocha huyo anadaiwa taji la ulaya ndani ya klabu hiyo ili kuingia kwenye vitabu vya historia kwenye klabu ya Manchester City kwani Ppe akiiwezesha klabu hiyo kubeba taji la ulaya anakua kocha wa kwanza kufanya hivo klabuni hapo.GuardiolaTaarifa za Guardiola kubakia klabuni City ni habari mbaya kwa vilabu vyote nchini Uingereza kutokana na utawala ambao ameuweka kwenye ligi hiyo kwani ndani ya miaka sita kwenye ligi hiyo tayari ameshatwaa mataji manne.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa