Kibu Denis Amvutia Vieira Mazoezini

Wakati Simba ikiwa bado huko Dubai kwa mualiko wa wiki moja kutoka kwa Rais wa heshima wa klabu hiyo Mohamed Dewji imeendelea na mazoezi na Kibu Denis amemvutia kocha mpya Roberto Vieira na kumpatia zawadi.

 

Kibu Denis Amvutia Vieira Mazoezini

Kibu Denis ambaye amekuwa hana mwendelezo mzuri wa kiwango na kufanya mashabiki wengi wa Simba kuanza kumjadili kuwa ameshuka amemvutia kocha huyo wa Kibrazili kutokana na kiwango ambacho amekionyesha.

Kocha amesema hiyo ni kawaida yake kumpatia mchezaji zawadi ambaye amefanya vizuri hivyo wachezaji wanatakiwa kuonyesha ubora wao.

Mchezaji huyo ndiye aliyekuwa kinara wa mabao wa Simba msimu uliopita akifanikiwa kupachika mabao 8 huku klabu hiyo ikimaliza nafasi ya pili na ubingwa wao wakishindwa kuutetea mbele ya watani wao Yanga.

Kibu Denis Amvutia Vieira Mazoezini

Wekundu wa Msimbazi watacheza mechi mbili za kirafiki kabla ya kurejea Dar es salaam kwa mchezo dhidi ya Mbeya City. Waatanza kesho dhidi ya Al Dhafra na siku ya tarehe 15 watamenyana dhidi ya CSKA Moscow  ili kujiweka fiti.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.