Wakati Simba ikiwa bado huko Dubai kwa mualiko wa wiki moja kutoka kwa Rais wa heshima wa klabu hiyo Mohamed Dewji imeendelea na mazoezi na Kibu Denis amemvutia kocha mpya Roberto Vieira na kumpatia zawadi.
Kibu Denis ambaye amekuwa hana mwendelezo mzuri wa kiwango na kufanya mashabiki wengi wa Simba kuanza kumjadili kuwa ameshuka amemvutia kocha huyo wa Kibrazili kutokana na kiwango ambacho amekionyesha.
Kocha amesema hiyo ni kawaida yake kumpatia mchezaji zawadi ambaye amefanya vizuri hivyo wachezaji wanatakiwa kuonyesha ubora wao.
Mchezaji huyo ndiye aliyekuwa kinara wa mabao wa Simba msimu uliopita akifanikiwa kupachika mabao 8 huku klabu hiyo ikimaliza nafasi ya pili na ubingwa wao wakishindwa kuutetea mbele ya watani wao Yanga.
Wekundu wa Msimbazi watacheza mechi mbili za kirafiki kabla ya kurejea Dar es salaam kwa mchezo dhidi ya Mbeya City. Waatanza kesho dhidi ya Al Dhafra na siku ya tarehe 15 watamenyana dhidi ya CSKA Moscow ili kujiweka fiti.