Je Cloutus Chota Chama Ni wa Kucheza Dakika 33?

Ligi kuu ya NBC ilipigwa jana kwa mchezo mmoja ambao ulikuwa ni wa Simba dhidi ya Mbeya City katika Dimba la Mkapa huku Chama dakika 33 zikimtosha na kufanyiwa mabadiliko.

 

Je Cloutus Chota Chama Ni wa Kucheza Dakika 33?

Mchezo huo ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 3-2 dhidi ya Mbeya huku kukiwa na maswali mengi juu ya mabadiliko aliyofanyiwa Chama na kuingia Kibu Denis katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Licha ya Chama kutoa pasi ya bao la kwanza kwa Saido Ntibanzokiza dakika ya 10 ya mchezo kocha Roberto aliona ni sahihi kumtoa kiungo huyo kutoka Zambia huku mashabiki wa Simba wakiwa hawajaridhishwa kabisa na mchezaji huyo kutolewa.

Ndani ya dakika mbili baada ya bao hilo Mbeya City walisawazisha bao hilo kupitia kwa Ngodya pasi ya bao ikitoka kwa Kihimbwa ambaye amekuwa akiwasumbua Msimbazi toka akiwa Mtibwa Sugar.

Je Cloutus Chota Chama Ni wa Kucheza Dakika 33?

Ntibanzokiza amepachika mabao mawili hapo jana moja likiwa kwa penalti huku Sakho akifunga la tatu, Manula akifanya uzembe na kuruhusu bao la pili kwenye mchezo wa jana. Kadi nyekundu inatoka kwa beki wa timu ya Mbeya baada ya kumchezea Mohamed Hussen na kucheza kuwa pungufu.

Mijadala inaendelea kocha Mbrazil aliona nini kumtoa Chama ambaye ndiye injini ya Simba na pia ndiye kinara wa pasi za mabao ya Ligi kuu ya NBC, na majibu ya mwalimu ni kwamba anataka timu icheze na ishinde.

Je Cloutus Chota Chama Ni wa Kucheza Dakika 33?

Ni mechi yake ya kwanza na ameshinda huenda mchezo hukuwa mzuri kutokana na uchovu lakini bado mashabiki hawakuridhishwa na kutolewa kiungi huyo fundi hapa Tanzania.

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.