Yanga Kumkaribisha Ruvu Shooting Hapo Kesho

Klabu ya Yanga baada ya kupata ushindi mwembamba mechi iliyopita, kesho wanatarajia kushuka dimbani kwa Mkapa kukiwasha dhidi ya Ruvu Shooting ya Mbwana Makata.

 

Yanga Kumkaribisha Ruvu Shooting Hapo Kesho

Yanga ambao ni vinara wa ligi mpaka sasa wameshinda mechi zao 17 kati ya 20 walizocheza, wakitoa sare mbili na kupoteza mchezo mmoja huku wakijivunia pointi 53 kibindoni.

Klabu hiyo ambayo ipo chini ya kocha mkuu Nasredine Nabi imeshinda mechi zake saba mfululizo huku kwenye hizo mechi saba ni mechi moja tuu ambayo waliruhusu nyavu zao kutikiswa ambayo ni dhidi ya Azam.

Yanga Kumkaribisha Ruvu Shooting Hapo Kesho

Wakati kwa uapande wa Ruvu Shooting wao wapo nafasi ya 15 ambayo ni ya pili kutoka mwisho kwenye msimamo, wakiwa wamevuna pointi 14, ushindi michezo mitatu, sare tano na kupoteza mara 12.

Ruvu mara ya mwisho kushinda ilikuwa Septemba 29, huku wakienda mechi 15 bila kupata pointi tatu kwenye ligi licha ya kumtangaza Mbwana Makata kama kocha mkuu wa timu hiyo.

Yanga Kumkaribisha Ruvu Shooting Hapo Kesho

Je Ruvu anaweza kupata hata pointi hapo kesho mbele ya Mabingwa watetezi wa Ligi Young Africans?.

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.