Wakati wa mechi ya Simba SC dhidi ya Mbeya City kwenye dimba la Mkapa kumalizika kwa Mnyama kupata ushindi mgumu 3-2, jambo lililozua taharuki kwa mashabiki ni Chama kufanyiwa mabadiliko dakika ya 30 tu na kocha wa timu hiyo Robertinho. Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet.

Afisa Habari wa Simba SC Ahmed Ally amesema kuwa kiutawala wamefurahia kuona Kocha amefanya maamuzi magumu. Meridianbet inakupa uwezo wa kubashiri mubashara na odds kubwa juu.
“Watu wote waliokuwa uwanjani na waliokuwa wanatazama kupitia TV tulishtuka kuona Kocha Robertinho anamtoa Chama!”
“Baada ya kushtuka kuna watu ambao tukaamua kusubiri kuona Kocha anataka kufanya nini halafu wapo waliosema huyu Kocha hatufai! Waliosema huyu Kocha hatufai hadi sasa hivi wameshikilia msimamo huo.”
“Tulioamua kusubiri kuona kocha atafanya nini alitujibu palepale uwanjani, baada ya muda mfupi tukaona kwa nini aliamua kufanya mabadiliko yale.”
“Maamuzi aliyoyafanya ni kwa maslahi ya timu, kwa jicho lake la kiufundi aliona pamoja na ubora wote wa Chama lakini kwenye mchezo ule alihitaji mtu mwingine.”
“Kiutawala sisi tumefurahi kuona tuna mwalimu ambaye anaweza kufanya maamuzi magumu! Kwenye maisha huwezi kufanikiwa kama huwezi kufanya maamuzi magumu.”

Baada ya mabadiliko ya kumtoa Chama na kumuingiza Pape Sakho ambaye alikuja kubadilisha mchezo na baadae alifunga bao la ushindi kwa Simba kwa shuti kali nje ya 18, ni baada ya Saidoo Ntibazonkiza kumgasi kwa nguvu mchezaji wa Mbeya City na kumpora mpira kisha Sakho akapiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango. Mechi zote za Bongo zina odds kubwa meridianbet, Bashiri hapa.

