Klabu ya Real Madrid leo itashuka dimbani kumenyana na klabu ya Villarreal ambapo mchezo huo unatafsiriwa kama mchezo wa kisasi baina ya timu hizo kwenye kombe la mfalme.
Klabu ya Real Madrid itakua ina nafasi ya kulipiza kisasi leo dhidi ya klabu ya Villarreal katika mchezo wa kombe la mfalme, Klabu hiyo ilipoteza mchezo wake wa mwisho wa ligi kuu ya Hispania dhidi ya Villarreal hivo klabu hiyo inaweza kutumia mchezo wa leo kulipiza kisasi.Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Hispania na ligi ya mabingwa ulaya wanakwenda katika mchezo huu pia wakiwa na maumivu makali ya kufungwa katika mchezo wa fainali ya kombe la Spanish Super Cup dhidi ya klabu ya Barcelona kwa mabao matatu kwa moja.
Real Madrid leo itaendelea kumkosa kiungo wake raia wa kimataifa wa Ufaransa Aurellien Tchouameni ambaye anaandamwa na majeraha, Kiungo huyo alikosekana katika mchezo wa fainali ya Spanish Super Cup dhidi ya klabu ya Barcelona pia.Klabu ya Villarreal pia nayo ina nafasi ya kuendelea kulinda rekodi yao dhidi ya klabu ya Real Madrid ya kutokupoteza mchezo katika uwanja wao wa nyumbani, Villarreal wamekua kwenye kiwango kizuri sana pale ambapo wanakua wakicheza na mabingwa watetezi wa hao wa ligi kuu ya Hispania na mchezo huo unatarajiwa kua wenye ushindani mkubwa.