Aliyekua Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Jesse Lingard ametia chumvi kidonda baada ya kusema klabu hiyo ipo nyuma sana kwenye suala la miondombinu ukilinganisha na vilabu kama Manchester City na Tottenham.
Lingard ambaye anakipiga katika klabu ya Nottingham Forest kwasasa amesema hayo baada ya miezi miwili nyuma aliyekua nyota wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo alisema kua klabu ya Manchester ipo nyuma sana kwenye suala miundombinu, Hivo hii inaonesha kweli klabu iyo ina tatizo kwenye suala la miondombinu.
Mchezaji huyo anasema ukiangalia klabu kama Manchester City au Tottenham zenyewe zimejiimarisha sana nje ya kiwanja kwenye suala la miondombinu, Huku klabu yake ya zamani ya Manchester United ikiwa imeachwa mbali sana na vilabu hivo haswa ikija suala la vifaa vya mazoezi.
Mchezaji Jesse Lingard pia kwenye mahojiano yake alifunguka kua msimu uliomalizika alifikia hatua ya kutumia pombe ili aweze kua sawa kutokana na kipindi kigumu ambacho alikua anapitia ndani ya klabu ya Manchester United kwenye msimu wa 2021/22.
Jesse Lingard amekua ndani ya klabu ya Manchester United kwa miaka 22 kabla ya kuondoka kwa uhamisho huru ndani ya msimu huu kuelekea klabu ya Nottingham Forest, Ameweka wazi alikua halali bila kunywa pombe kutokana na wakati mgumu aliokua anapitia ndani ya klabu hiyo na hiyo ni kutokana na kukosa nafasi na kufikia hatua hadi ya kutolewa kwa mkopo kwenda klabu ya West Ham.

