Simba Kusaka Pointi 3 kwa Mkapa Leo

Klabu ya Simba inatarajia kusguka dimbani hii leo majira ya saa 1:00 usiku kukiwasha dhidi ya Singida Big Stars kwenye mchezo wa Ligi kuu ya NBC wa raundi ya 22 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

 

Simba Kusaka Pointi 3 kwa Mkapa Leo

Simba ambao wapo nafasi ya pili, wamecheza michezo yao 21, wameshinda 15, sare tano na wamepoteza mchezo mmoja hadi sasa wakijikusanyia pointi 50 na ndiyo timu inayoongoza kwa kufunga mabao mengi.

Wakati kwa upande wa Singida Big Stars wao wapo nafasi ya nne, baada ya kushinda michezo yao 13, sare zikiwa ni nne, na kupoteza mara nne huku wakiwa na pointi 43 kwenye msimamo.

Simba Kusaka Pointi 3 kwa Mkapa Leo

Mechi iliyopita ya ligi vijana wa Msimbazi walipata ushindi mwembamba, halikadhalika kwa Walima Alizeti nao walipata ushindi mwembamba. Mchezo wa kwanza walivyokutana walitoshana nguvu kwa kufungana bao moja moja huku mnyama akitokea nyuma.

Je hiii leo nani ataondoka na ushindi, huku Simba akihitaji ushindi aweze kumfukuzia Yanga ambaye anapishana nae pointi 6. Deus Kaseke anakosekana kwenye mchezo wa leo. Pluijm atafanya nini?

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.