Mbappe Kuwakosa Bayern Munich

Mshambuliaji wa klabu ya PSG kylian Mbappe inaelezwa atakua nje ya uwanja kwa muda wa takribani wiki tatu hivo kumfanya kuukosa mchezo muhimu wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Bayern Munich.

Mshambuliaji Kylian Mbappe alionekana kuchechemea katika mchezo ambao PSG walipata ushindi wa mabao matatu kwa moja hapo, Lakini hapo mwanzo ilionekana kua jeraha hilo haliwezi kua na tatizo kubwa sana lakini mpaka sasa inaoneakana atakua nje kwa muda.MbappeMshambuliaji wa huyo ni wazi ataukosa mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya klabu ya Bayern Munich katika hatua ya 16 bora utakaochezwa mwezi huu wapili kutokana na taarifa ambayo imeeleza kua mchezaji huyo atakua nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu.

Mbappe atakua nje kwa muda wa wiki tatu ambapo atakosa mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora dhidi ya Bayern Munich kwenye ligi ya mabingw abarani ulaya, Lakini taarifa nzuri ni kua mchezaji huyo atakosekana katika mchezo wa awali tu lakini mchezo wa marudiano utamkuta staa huyo akiwa tayari amerejea.MbappeKukosekana kwa mshambuliaji Kylian Mbappe ndani ya klabu ya PSG kwa muda wa wiki tatu ndani ya klabu hiyo ni pengo kubwa licha ya klabu hiyo kua na mastaa kadhaa kama Messi, na Neymar lakini umuhimu wa mchezaji huyo ni mkubwa sana ndani ya timu hiyo, Zaidi kwenye mchezo muhimu dhidi ya Bayern Munich.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.