Andre Ayew Ajiunga Nottingham Forest

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Al Sadd inayoshiriki ligi kuu nchini Qatar Andre Ayew amefanikiwa kujiunga na klabu ya Nottingham Forest inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza kwa mkataba wa muda wa miezi sita.

Andre Ayew mshambuliaji huyo wa zamani kutoka klabu ya Swansea City amefanikiwa kujiunga na klabu hiyo ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kuondoka nchini humo kwa misimu kadhaa, Lakini baada ya miaka kadhaa ameweza kurejea tena nchini humo.andre ayewMshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ghana amekua miongoni mwa wachezaji waliozitumikia timu nyingi ndani ya ligi kuu ya Uingereza kwani Nottingham Forest inakua klabu ya tatu kuitumikia nchini humo ambavyo ni vilabu vya Swansea, West Ham, na sasa Nottingham.

Andre Ayew sasa ataitumikia klabu ya Nottingham Forest kwa muda wa miezi sita akiwa kama mchezaji huru kutoka ndani ya klabu ya Al Sadd. Kuna uwezekano mkubwa mchezaji huyo akaendelea ndani ya timu hiyo kama akifanya vizuri ndani ya timu hiyo.andre ayewMshambualiaji Andre Ayew amekua akifanya vizuri katika vilabu tofauti tofauti na ndio sababu kubwa ya kuendelea kupata timu katika ligi kuu ya Uingereza, Lakini pia mshambuliaji huyo anakwenda kuungana na kocha wake wa zamani ndani ya klabu ya Swansea kwasasa akiitumikia Nottingham Forest Steve Cooper.

 

Acha ujumbe