Ghana OUT AFCON 2021.

 

Timu ya Taifa ya Ghana ( Black Stars ) imeondolewa rasmi kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 na timu ya taifa ya Comoros katika mchezo wa mwisho wa Kundi C kwa kipigo cha goli 3-2 katika mchezo uliopigwa jana Jumanne Januari 18.

 

Ghana ambao ni washindi wa Kombe la Afcon mara nne wametolewa na timu ambayo ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano hiyo mikubwa ngazi ya mataifa Afrika-AFCON.

El Fardou Ben Nabouhane aliipa uongozi Comoros mapema ikafuatiwa na kadi nyekundu ya moja kwa moja iliyotolewa kwa mchezaji mashuhuri Andre Ayew.

Ahmed Mogni aliongeza bao la pili kwa wageni wa michuano Comoros kabla ya Ghana Black Stars kupambana na kurudisha bao hizo na matokeo kuwa 2-2.

Dakika za jioni Ahmed Mogni alifunga goli la tatu kwa Comoros timu ya Visiwani ambayo inashika nafasi ya 132 kwenye viwango vya Fifa bao ambalo limevunja rekodi iliyodumu tangu mwaka 2006.

Ghana ilianza kwa matokeo ya kusuasua kwenye mashindano haya ambapo walianza na kipigo cha kufungwa goli 1-0 na Morocco kabla ya kutoa sare ya bao 1-1 na Gabon.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.