Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Paris St-Germain wanafanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 28, na kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast Franck Kessie, 25, kutoka Manchester United na AC Milan.

Tetesi zinasema, Roma Jose Mourinho, 58 amekanusha za kujiunga na Everton baada ya madai kuibuka kuwa ni mmoja wa makocha wanaopigiwa upato kuchukua nafasi ya Rafael Benitez.

Tetesi zinasema, Newcastle wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Adana Demirspor na Italia Mario Balotelli, 31, kulingana na rais wa klabu hiyo ya Uturuki Murat Sancak.

 

Arsenal wamepiga hatua kumsajili kiungo wa kati wa Brazil na Juventus Arthur Melo, 25, baada ya klabu yake ya Itaila kuanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Lyon wa miaka 24 Mbrazil Bruno Guimaraes kuchukua nafasi yake.

Arsenal wamepata pigo katika juhudi zao za kumsaka mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic, 21, baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia kudai anataka kujiunga na Juventus pekee.

Tottenham bado wanajaribu kumsaini winga wa Uhispania Adama Traore Januari hii licha ya kocha wa Wolves Bruno Lage kumshinikiza kiungo huyo wa miaka 25 kusalia katika klabu hiyo hadi mwisho wa msimu.

Mshambuliaji wa Croatia Ivan Perisic hataondoka Inter Milan mwezi huu wa Januari licha ya tetesi zinazomhusishana Chelsea. Mkataba wa winga huyo wa miaka 32-unakamilika mwezi Juni lakini Inter inapanga kurefusha mkataba.

 

Dybala Juventus
Paulo Dybala

Tetesi zinasema, Inter Milan pia wanafuatilia hali ya Paulo Dybala,28, Juventus huku mkataba wa mshambuliaji huyo wa Argentina ukielekea kukamilika msimu huu wa joto.

Barcelona na Bayern Munich wanaongoza katika mbio za kumsaka beki wa Chelsea Andreas Christensen, 25, huku mlinzi huyo wa Denmark akikataa ofa za klabu za Uingereza kwa heshima ya the Blues.

Barcelona wana mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 22, kutoka Real Sociedad wakishindwa kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.