Australian Open: Osaka vs Brengle, Burudani!

Mchezo wa mzunguko wa pili (kwa wanawake) umemalizika kunako Australian Open. Naomi Osaka vs Madison Brengle ni burudani!

Osaka ameonesha ukomavu na ustahimilivu uliojaa uwezo mkubwa wa kupiga mipira yenye madhara kwa mpinzani wake. Seti ya kwanza ni kielelezo thabiti cha uwezo wa Naomi Osaka kwenye ulimwengu wa tenesi.

Takwimu za Mchezo; Osaka vs Brengle.

Akiwa ndio bingwa mtetezi wa Australian Open. Osaka aliongoza kwa matokeo ya 6-0 katika seti ya kwanza kabla ya Brengle kurejea mchezoni kwenye seti ya pili.

Burudani halisi ya mchezo wa tenesi ilionekana kwenye seti ya pili ambapo, Brengle alionesha uwezo wake wa matokeo ya piga ni kupige. Mmarekani huyu aliongoza kwa matokeo ya 2-1 kabla ya Osaka kulipa na kuwa 2-2.

Naomi Osaka

Dakika chache baadae, matokeo yakawa 3-3 kabla ya Osaka kuongeza juhudi na kuonesha ubora wake mpaka kumaliza mchezo kwa matokeo ya 6-4.

Osaka atachuana na Amanda Anisimova katika mchezo wa mzunguko wa 3. Huu ni mchezo ambao unawakutanisha wachezaji wawili ambao hawajapoteza mchezo wowote kabla na baada ya mashindano ya Australian Open kuanza kwa mwaka 2022.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe