Kiungo mpya wa klabu ya Manchester United Marcel Sabitzer ameahidi makubwa ndani ya klabu hiyo pindi atakapoanza rasmi kuanza kuitumikia timu hiyo.
Kiungo Sabitzer ambaye amejiunga na klabu ya Manchester United akitokea ndani ya klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani kwa mkopo, Kiungo huyo wakati akifanya mahojiano kwa mara ya kwanza baada ya kujiunga na timu hiyo amesema kua atajitoa kadri awezavyo kuhakikisha timu hiyo inapata matokeo.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Austria inafahamika amejiunga na timu hiyo ili kuziba nafasi ya kiungo wa klabu ya Manchester United Christian Eriksen ambaye amepata majeraha na atakua nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu, Hivo kiungo huyo kutoka Bayern Munich ndio mwalimu Erik Ten Hag alimuona anafaa kuvaa viatu vya Eriksen.
Kiungo Marcel Sabitzer pia amezungumza juua ya kiu yake ya kucheza kwenye dimba la Old Trafford ambapo alishawahi kucheza mara moja akiwa na klabu ya Rb Leipzig, Lakini ameweka wazi kua aatamani sana kucheza kwenye dimba hilo kwani ni heshima kubwa kwakua Manchester United ni klabu kubwa.
Kiungo huyo pia anaeleza kilichomleta ndani ya klabu ya Manchester United sio kitu kingine zaidi ya kushinda mataji ndani ya klabu hiyo,Lakini Marcel Sabitzer hakusita kueleza kua furaha yake ilikua kujiunga na klabu ya Manchester United akitokea Bayern Munich na kwasasa ana furaha kubwa ndani ya timu hiyo.

