Morrison Nje Miezi Miwili

Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Ali Kamwe amethibitisha mchezaji wao Bernard Morrison atakuwa nje kwa muda wa miezi miwili baada ya kupata majeraha ya nyonga.

 

Morrison Nje Miezi Miwili

Mchezaji huyo ambaye ametoka kuonywa kutokana na kuchelewa kurudi kambini baada ya ligi kusimama kwaajili ya kupisha michuano ya Mapinduzi yaliyokuwa yanafanyika kule Zanzibar atakosa michezo ya awali ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya US Monastir ya Tunisia February 12.

Uwepo wa Morrison kwenye kikosi cha Nabi ilikuwa inamfanya kocha huyo kuwa na washambuliaji wengi kwenye eneo hilo la mbele ambalo linaongozwa na Fiston Mayele mwenye mabao 15.

Morrison Nje Miezi Miwili

Licha ya kutangazwa kuwa ameumia mchezaji huyo hajacheza mechi kadhaa za mabingwa hao watetezi wa ligi kuu msimu uliopita, na bado anaendelea kuwa nje tena kutokana na majeraha hivyo inawezekana ikawa ni pigo kwa kocha mkuu wa kikosi cha Yanga.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.