Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara inaendelea hii kwa michezo kadhaa ambapo mchezo wa mapema majira ya saa 8:00 mchana ambapo Ihefu atakiwasha dhidi ya Mbeya City.

Timu hizi zote zinatokea Mbeya na timu ambayo inajitahidi kwenye ligi ni ya Mbeya ambapo mpaka sasa ipo nafasi ya 9 baada ya kucheza michezo yao 21, wakishinda mechi zao 5, sare 9 na kupoteza michezo 7 alama 24.
Wakati kwa Ihefu wao hali yao sio nzuri sana kwani wapo nafasi ya 12, kwenye msimamo wakiwa wameshinda mechi zao 7, sare 2, na kupoteza michezo yao 12 na kujikusanyia pointi 23.

Timu zote zimetoka kupata pointi 3 kwenye michezo yao iliyopita huku mchezo huu wa leo kila timu ikihitaji alama ili iweze kusogea nafasi inayofuata.
Mechi ya mwisho ya mwisho kukutana timu hizi, walitoshan nguvu kwa kufungana bao 1-1. Je hii leo inaweza kuwa sare nyingine? Au kuna timu itaondoka kifua mbele. ODDS KUBWA zipo Meridianbet.

