Mechi nyingine inayotarajiwa kutimua vumbi ni kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Ihefu ambao wametoka kupoteza mchezo wao uliopita kwa Mkapa.

Tanzania Prisons nao wametoka kupoteza michezo miwili mfululizo huku mchezo wa kesho wakihitaji ushindi ili waweze kutoka katika nafasi waliyopo ya 11 kwani ni mbaya endapo ataendelea kupata matokeo hayo.
Ihefu wapo nafasi ya 13, baada ya kucheza michezo 20 kwenye ligi wakivuna alama zao 20, wakiwa wameshinda michezo sita, sare mbili na kupoteza michezo 12 ambayo ni mingi kwa timu ambayo haitaki kushuka daraja.

Prisons wao wameshinda michezo mitano sare sita na kupoteza michezo tisa wakijikwamulia pointi 21 huku tofauti yao ikiw ani pointi moja tu, hivyo yoyote atakayeshinda atapanda kutoka alipo.
Mechi ya mwisho kukutana timu hizi mbili, walitoka sare ya kufungana bao 1-1. Je kesho nani kuondoka mbabe katika uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 jioni.

