La Gazzetta dello Sport inadai Inter tayari wametoa ofa ya kumsajili Marcus Thuram anayelengwa na Barcelona na Chelsea kama mchezaji huru msimu wa joto.

The Nerazzurri ni wapenzi wa muda mrefu wa mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ufaransa, ambaye anaona mkataba wake na Borussia Monchengladbach unamalizika mwishoni mwa msimu.
Mkurugenzi wa Inter, Beppe Marotta alikuwa kwenye mazungumzo na timu hiyo ya Bundesliga kwenye dirisha la usajili la Januari, akitarajia kumnyakua mchezaji huyo kwa bei nafuu. Alikuwa amempa mshambuliaji huyo mkataba wa €5m kwa mwaka, ambao, kulingana na Gazzetta, bado upo mezani.

Thuram sasa yuko huru kusaini mkataba wa awali wa kandarasi na klabu nyingine yoyote, akijiunga kama mchezaji huru mwishoni mwa kampeni. Hata hivyo, mtoto wa mlinzi maarufu wa Serie A, Lilian haonekani kuwa na haraka ya kuamua hatima yake ijayo.
Chelsea imetajwa kuwa miongoni mwa klabu zinazomtaka Thuram, huku Gazzetta ikidai Barcelona, Atletico Madrid na Bayern Munich wanafuatilia kwa karibu hali hiyo lakini bado hawajatoa ofa.

Thuram mwenye miaka 25, amefunga mabao 13 katika mechi 21 katika mashindano yote msimu huu.

