Klabu ya Namungo itakuwa ugenini hii leo kusaka pointi 3 mbele ya vijana wa Mecky Mexime Kagera Sugar katika dimba la Kaitaba majira ya saa 1:00 usiku.

Namungo wametoka kudondosha pointi zote tatu wakiwa ugenini dhidi ya vinara wa Ligi Yanga na leo wapo ugenini dhidi ya Walima Miwa ambapo wao nao mechi iliyopita walitoka kutoa sare mechi yao iliyopita.
Wauaji wa Kusini wanashikilia nafasi ya 6 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo yao 22 wakiwa wameshinda michezo yao nane, sare tano na wamepoteza mara tisa hadi sasa alama 29 kibindoni.

Mexime na vijana wake wamekusanya pointi zao 26 baada ya mechi 22 walizoingia dimbani nyumbani na ugenini, wakishinda michezo sita, sare nane na kupoteza michezo yao nane.

