Ligi ya Mabingwa Barani Afrika itaendelea tena hii leo kwa michezo kadha wa kadha, ambapo kwa Mkapa utapigwa mchezo kati ya Simba dhidi ya Raja Casablanca ya nchini Morocco.

Simba walipoteza mechi yao ya kwanza kwenye hatua ya makundi, na hii ni mechi ya pili ambayo wanatarajia kupata pointi tatu dhidi ya timu kubwa Afrika Raja ambaye ametoka kumfunga Vipers mechi ya kwanza.
Kwenye kundi C mnyama yupo nafasi ya tatu, lakini pia itamkosa kiungo wake Sadio Kanoute ambaye alipewa kadi za njano mbili mfululizo lakini kuna uwezekano wa kumchezesha Saido Ntibanzokiza.

Je Roberto na timu yake wana nafasi gani hii leo, pointi 3 watazipata? au Raja anaweza kumzuia mnyama kuibuka mbabe?

