Serie A nayo ilikuwa ya moto sana wikendi hii kueleka mwaisho wa msimu ambapo, Inter Milan walirudishwa chini baada ya kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa, wakiangukia kwenye kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya mabingwa Napoli.

Inter walipunguzwa hadi wachezaji 10 pale Roberto Gagliardini alipotolewa nje kwa kadi nyekundu kabla ya muda wa mapumziko na Andre-Frank Zambo Anguissa kuiweka Napoli mbele katikati ya kipindi cha pili.
Romelu Lukaku alisawazisha bao huku wakiwa wachezaji 10 zikiwa zimesalia dakika nane kabla ya mechi kumalizika lakini Napoli walijibu kwa msisitizo kwa mabao ya Giovanni Di Lorenzo na Gianluca Gaetano.

Inter walishuka hadi nafasi ya nne nyuma ya Lazio, ambao waliilaza Udinese 1-0 kwa mkwaju wa penalti wa Ciro Immobile.
Torino na Fiorentina zilitoka sare ya 1-1 huku wapambanaji Lecce na Spezia wakilazimika kuambulia pointi moja kila mmoja katika sare ya 0-0.

