Inter Milan Yatawala Timu Bora ya Wiki Uefa

Klabu ya Inter Milan imetawala timu bora ya wiki ya michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya yaani Uefa Champions League baada ya michezo ya nusu fainali kupigwa ndani ya wiki siku ya Jumanne na Jumatano.

Inter Milan wamefanikiwa kuingiza wachezaji tisa kwenye kikosi cha wiki cha ligi ya mabingwa ulaya baada ya timu hiyo kucheza kwa kiwango bora sana katika mchezo wao wa nusu dhidi ya mahasimu wao klabu ya Ac Milan baada ya kupata ushindi wa mabao mawili kwa bila katika mchezo uliopigwa jana.inter milanVijana wa Simeone Inzaghi jana walifanikiwa kupata matokeo ya ushindi dhidi ya Ac Milan katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa ulaya, Kutokana na kiwango kikubwa walichoonesha Nezzazuri katika mchezo huo imesaidia kutoa wachezaji wengi kwenye kikosi cha wiki cha ligi ya mabingwa ulaya.

Inter Milan imefanikiwa kutoa wachezaji tisa ikiwa kila eneo uwanjani imetoa mchezaji kuanzia kwa golikipa , Mabeki watano, viungo wawili, pamoja mshambuliaji mmoja hii imeonesha ni kwa namna gani Nezzazuri wamecheza kwa kiwango kikubwa katika nusu fainali ya kwanza dhidi ya mahasimu zao Ac Milan.inter milanWachezaji wa Inter Milan walioingia kwenye timu hiyo ni golikipa Andre Onana, mabeki Denzel Dumfries, Dimarco, Acerbi,Bastoni, na Matteo Darmian, viungo ni Mikhytaryan, na Calhanoglu, mshambuliaji aliyeingia ni Edin Dzeko ambaye alifunga goli katika mchezo wa jana dhidi ya Ac Milan.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.