Simeone Inzaghi Awaonya Vijana Wake Baada ya Ushindi

Kocha wa klabu ya Inter Milan Simeone Inzaghi amewaonya wachezaji baada ya ushindi wa mabao mawili kwa bila katika mchezo wa nusu fainali wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Ac Milan na kuwaambia bado kazi haijaisha.

Inter Milan walifanikiwa kupata ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya mahasimu wao klabu ya Ac Milan mabao ya Edin Dzeko na Henrick Mikhytaryan yaliipa Inter ushindi, Lakini Simeone Inzaghi anasema wachezaji wake hawatakiwi kuona mechi imemalizika na wameshatinga fainali.simeone inzaghiKocha huyo akiongea na waandishi wa habari amesema bado wana kazi ya kufanya kwani kuna mchezo wa marudiano ambao utapigwa Jumanne ya wiki inayofuata, Hivo wachezaji wake wanatakiwa kua tayari kwakua kazi haijaisha pamoja na kujua kua wako mbele kwa mabao mawili mbele ya wapinzani wao.

Kocha Simeone Inzaghi pia alitoa pongezi kwa wachezaji wake kwa namna walivyocheza katika mchezo wa jana na kusema kile alichowaagiza ndicho ambach walikitekeleza, Kwakua wachezaji wake walicheza vizuri na kutokuacha nafasi yeyote kwa wapinzani kuweza kuwadhuru.simeone inzaghiKocha Simeone Inzaghi alisisitiza kua kazi bado haijamalizika lakini kama wakifanikiwa kwa kiwango ambacho wamekionesha katika mchezo huo basi watakua sehemu nzuri, Wakati huohuo kocha wa Ac Milan Stefano Pioli yeye anasema walikua na mechi mbaya siku ya jana lakini watahakikisha wanarudi kwenye mstari katika mchezo wa marudiano.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.