Skudu Aahidi Makubwa Yanga

Winga mpya wa Yanga, Skudu Makudubela amesema kuwa anaamini Yanga ya msimu ujao itaenda kuwashangaza watu kwa kupata mafanikio makubwa ambayo anaamini kuwa inatokana na kiu ya mafanikio ambayo wao kama wachezaji wanayo.

 

Skudu Aahidi Makubwa Yanga

Skudu ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga, kwenye mchezo dhidi ya Kaizer Chief winga huyo alifanikiwa kucheza kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza ambacho alifanikiwa kuwaonyeshea mashabiki wa Yanga uwezo mzuri na kumshangilia.

Skudu alisema kuwa: “Nafurahi kwa jinsi ambavyo nimepokelewa ndani ya Yanga kuanzia siku ya kwanza mpaka kwenye siku ya Wananchi, naamini kuna deni kubwa sana kwa Wananchi.”

Kuanzia mapokezi, utambulisho kwa wachezaji na mpaka ushindi ambao tuliupata kwenye mchezo wetu ni jambo la furaha na mwanzo mzuri kwangu ndani ya timu hii kubwa Afrika. Alisema mchezaji huyo

Skudu Aahidi Makubwa Yanga

Mashabiki wa Yanga wanapenda mpira jambo ambalo naliona ni zaidi ya familia kuicheza timu hii na niwaambie tu kuwa msimu ujao tutapambana kwa ajili ya kuyapata mafanikio makubwa zaidi na kuweka historia nyingine. Alisema mchezaji huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.