Aliyekuwa kocha msaidizi wa Yanga Cedric kaze amewaaga rasmi mashabiki, wanachama na viongozi wa timu hiyo mara baada ya kuachana na timu hiyo.
Cedric Kaze atarudi nchini kwao Burundi kwenda kutafuta namna ya kujiunga na timu nyingine.Hapo awali Cedric kaze alikuwa kuna madai anaidai Yanga na kisha kuweka sintofahamu dhidi ya uongozi uliopo madarakani kisha baadaye akaitwa ili wamalizane na kisha wakae mezani waone kama anaweza kuendelea kuwepo kwenye benchi la ufundi.
Kaze alitakiwa yeye na kocha mwingine msaidizi kutoka Senegal aliyetangazwa lakini mara baada ya kutua hapa nchini na kumalizika kwa kikao basi kaze na Yanga wameshindwana na sasa kocha huyo hatakuwepo tena Bongo na mwenyewe amethibitisha kupitia Instagram yao