Sakho Rasmi Sasa Auzwa Ulaya

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba imekubaliana kwa pamoja kumuuza kiungo wake mshambuliaji Msenegali, Pape Ousmane Sakho kwenda moja ya klabu ya Ulaya na sasa wapo katika hatua za mwisho za kumuachia.

 

Sakho Rasmi Sasa Auzwa Ulaya

Kiungo huyo anatarajiwa kutimkia Klabu ya Quevilly Motropole inayoshiriki Ligi Daraja la Pili ya Ufaransa.

Msenegali huyo alijiunga na Simba katika msimu wa 2021-22 ambaye alitarajiwa kuwa mbadala wa Luis Miqquissone aliyerejea tena katika msimu huu.

Taarifa zinasema, Simba wamefikia makubaliano mazuri na klabu hiyo ya Quevilly Motropole kwa kununua mkataba wake wa mwaka mmoja ambao ameubakisha hapo Simba.

Sakho Rasmi Sasa Auzwa Ulaya

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa ndani ya wiki hii kuanzia leo Jumatatu itatangaza kuachana na kiungo huyo na kwenda kucheza huko Ufaransa.

Aliongeza kuwa kiungo hiyo kabla ya kuuzwa alihitajika na baadhi ya klabu za Afrika ikiwemo Raja Casablanca ya nchini Morocco ambazo alikataa ofa zao.

“Muda wowote uongozi wa Simba tutatangaza kuachana na Sakho ambaye amepata ofa nzuri Ulaya. Anakwenda huko Ulaya kwa kumuuza baada ya yeye mwenyewe kuomba auzwe huko kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya.”

Sakho Rasmi Sasa Auzwa Ulaya

“Kama uongozi tumeona ni bora tumuachie ahende huko, kwani mwenyewe ameonekana na msimamo wa kwenda kucheza Ulaya,” Alisema mtoa taarifa huyo.

Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally alizungumzia hilo kwa kusema kuwa: Sakho bado mchezaji wa Simba kwa sasa na taarifa zake zitatolewa kama kweli anataka kuondoka.”

Acha ujumbe