Leon Goretzka anawindwa na klabu za Italia, lakini inaaminika anapendelea kuhamia Arsenal majira ya joto.

Goretzka ataondoka FC Bayern Munich bure mara mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. Kwa mujibu wa Sport Witness, yuko tayari kukataa ofa kutoka klabu mbalimbali barani Ulaya ili kuhakikisha anajiunga na Arsenal.
Mkurugenzi wa michezo wa Bayern, Christoph Freund, alisema mwezi Januari: “Leon anajisikia nyumbani sana katika klabu hii na timu hii. Licha ya kupokea ofa nyingi nzuri, aliamua kubaki hadi mwisho wa msimu. Baada ya mazungumzo ya wazi na yenye kujenga, tumekubaliana kuwa atatafuta changamoto mpya majira ya joto.”
Itakuwa miaka nane akiwa Bayern miaka minane yenye mafanikio makubwa. Ataendelea kujitolea hadi mwisho wa msimu ili kushinda mataji zaidi.”
Kiungo huyo aliwahi kuhusishwa na kuondoka wakati wa dirisha la Januari, lakini aliamua kubaki ili kuheshimu mkataba wake na Bayern.


