Newcastle United wana uwezekano mdogo wa kufuzu kwa UEFA Champions League msimu ujao, jambo ambalo linaweza kusababisha wachezaji kuondoka kwa wingi majira haya ya joto huku Howe kibarua chake kikiwa cha moto.

Eddie Howe yuko chini ya presha kuokoa nafasi yake ya ukocha Newcastle, huku mustakabali wake wa muda mrefu ukiwa na mashaka kutokana na hali isiyoeleweka ndani na nje ya uwanja, kwa mujibu wa Daily Mail.
Magpies chini ya Howe wanapitia msimu wa kiwango cha chini na kwa sasa wako nafasi ya 12 wakielekea hatua za mwisho za msimu. Walipoteza nyumbani kwa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao Sunderland katika mechi iliyopita, matokeo yaliyopunguza matumaini yao ya kufuzu mashindano ya Ulaya.
Ingawa nafasi ya kumaliza kwenye UEFA Champions League ni ndogo, Newcastle bado wako pointi sita tu nyuma ya nafasi sita za juu huku zikiwa zimesalia mechi saba.
Hata hivyo, ukosefu wa soka la Champions League msimu ujao kutokana na msimu mbaya wa ndani na kuondolewa kwa jumla ya mabao 8-3 katika hatua ya 16 bora na FC Barcelona una maana kuwa nyota kadhaa wanatarajiwa kuondoka St. James’ Park majira haya ya joto.
Sandro Tonali aliwahi kuhusishwa na uhamisho wa siku ya mwisho kwenda Arsenal, lakini dili hilo halikufanikiwa. Hata hivyo, bado anafuatiliwa na vilabu vikubwa vya Ulaya, wakiwemo Arsenal, Manchester City na Real Madrid.


