Klabu ya Chelsea inaendelea kupitia kipindi kigumu chini ya kocha Liam Rosenior, huku changamoto za uwanjani na tetesi za uhamisho zikizidi kuongezeka ndani ya kikosi hicho.
Beki wa kushoto Marc Cucurella ameongeza presha kwa klabu hiyo baada ya kukiri wazi kuwa itakuwa vigumu kuikataa Barcelona iwapo watamfuata katika dirisha la usajili la majira ya joto.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Cucurella, ambaye alikulia katika akademi maarufu ya La Masia, alisema kuwa kurejea Barcelona ni jambo linalowezekana, ingawa uamuzi wake wa mwisho utazingatia zaidi familia yake.
“Barcelona ni sehemu muhimu ya maisha yangu ya soka, lakini maamuzi kama haya lazima yahusishe familia yangu pia,” alinukuliwa akisema beki huyo wa kimataifa wa Hispania.
Wakati huo huo, hali ndani ya Chelsea inaonekana kuwa tete zaidi kufuatia taarifa zinazoeleza kuwa kiungo mshambuliaji Cole Palmer anavutiwa na kujiunga na Manchester United, huku Enzo Fernández akitajwa kutamani kuhamia Real Madrid.
Mfululizo wa tetesi hizi unaongeza wasiwasi kwa mashabiki wa Chelsea, ambao wanahofia kupoteza nyota wao muhimu wakati klabu hiyo ikiwa bado inajijenga upya chini ya benchi jipya la ufundi.

