Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) limeruhusu kuingiza mashabiki uwanjani kwenye mchezo wa kufuzu kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na DR Congo utakaochezwa Novemba 11, 2021 uwanja wa Benjamin Mkapa.

CAF imeruhusu jumla ya mashabiki 30,000 pekee kuingia kuutazama mchezo huo utakaochezwa majira ya saa 10 jioni katika dimba la Mkapa, Jiji la Dar es salaam.
Shirikisho hilo limesisitiza mashabiki watakaohudhuria mchezo huo kufuata itifaki zote za kijikinga na Uviko-19 kwa kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuvaa barakoa.
Aidha pia TFF nayo imesisitiza mashabiki kufuata maelekezo waliyoyatoa CAF. Tayari Stars ipo kambini kwaajili ya michezo ya kufuzu kombe la Dunia nchini Qatar 2022.
Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.


