Kikosi cha Simba SC kitaingia kambini baada ya mazoezi ya leo jioni kujiandaa na mchezo wa nne wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya RS Berkane utakaopigiwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 10 jioni.

Simba SC wanajua umuhimu wa mchezo huo baada ya kupoteza katika mchezo wa kwanza, wanahitaji kupata alama tatu nyumbani ambazo zitawaweka katika nafasi nzuri kwenye kundi lao kuelekea kufuzu kucheza robo fainali ya mashindano hayo.
Tayari viingilio vya mchezo vimeshatangazwa mapema ili mashabiki wanunue tiketi kupitia kwenye mitandao na kwenye vituo.
Viingilio vya mchezo wa Simba SC vs RS Berkane vipo kama ifuatavyo:
Mzunguko Sh 3,000
VIP B na C Sh. 20,000
VIP A Sh 30,000
Platinum Sh 150,000
Uongozi wa Simba SC umetoa rai kwa mashabiki kununua tiketi zao mapema katika maeneo mbali mbali na mitandao ya simu ili kuepuka usumbufu siku ya mchezo.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


