Simba Fungu La Kukosa Kwa Mkapa Klabu Bingwa

Mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba SC na Petro de Luanda ya Angola ulimalizika kwa Wekundu wa Msimbazi kupokea kichapo cha bao 1-0 katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam jioni ya jana.

Simba, ambayo ilihitaji ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuendelea na mbio za kutinga robo fainali, ilijikuta ikicheza chini ya kiwango huku wageni kutoka Angola wakionyesha ubora mkubwa katika dakika nyingi za mchezo. 

Simba Fungu La Kukosa Kwa Mkapa Klabu Bingwa

Bao pekee lililoizamisha Simba SC lilifungwa na kiungo Mreno, Bernardo Oliveira Dias dakika ya 78 alipofumua shuti la umbali wa mita 20 ambalo lilimbabatiza beki raia wa Afrika Kusini, Rushine De Reuck na kubadili njia likimpoteza mwelekeo kipa namba moja Tanzania, Yakoub Suleiman Ali.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kuburuza mkia katika kundi lake, ikiwa nafasi ya nne. Petro de Luanda inabaki kileleni ikiwa na rekodi nzuri ya mchezo wake wa awali. Esperance de Tunis inashika nafasi ya pili huku Stade Malien ikibaki katika nafasi ya tatu.

Simba inatarajiwa kufanya marekebisho makubwa kabla ya michezo ijayo ili kufufua matumaini ya kupenya kwenye hatua ya mtoano, ingawa safari inaonekana kuwa ngumu.

Simba Fungu La Kukosa Kwa Mkapa Klabu Bingwa

Mechi nyingine ya Kundi D jana Espérance ililazimishwa sare ya bila mabao na Stade Malien ya Mali Uwanja wa Hammadi Agrebi, Tunisde Jijini Tunis nchini Tunisia.

Mechi zijazo Simba SC itasafiri kuwafuata Stade Malien Novemba 29 Uwanja wa Machi 26 Jijini Bamako nchini Mali, wakati Petro de Luanda wanarejea nyumbani kuwakaribisha Espérance de Tunis November 29. Uwanja wa Novemba 11 Jijini Luanda

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu CCM, Asha Baraka alisema, matokeo hayo siyo matokeo mazuri ambayo walikuwa wanayatarajia lakini wanakubalina kuwa lazima wajipange vema kwenye mechi zijazo kama wanataka kwenda robo fainali.

Simba Fungu La Kukosa Kwa Mkapa Klabu Bingwa

“Kiukweli mchezo ulikuwa mgumu sana kwetu na tumecheza na timu nzuri tofauti na ambavyo tulitarajia, wachezaji wetu wamejitahidi sana ingawa hatujapata matokeo mazuri.  Lakini lazima tukubali wenzetu walituzidi kwenye baadhi ya maeneo.

“Inabidi tujipange sasa kwa sababu kuna mchezo wa marudiano, tunapaswa kujipanga ili kwenda kushinda  kwenye mechi inayokuja ili tujiweke kwenye mazingira mazuri kwenye kundi letu. Kwa wanasimba wenzangu hawapaswi kukata tamaa, inabidi tuwatie moyo wachezaji wetu ili wafanye vizuri kwenye mechi zingine zinazokuja,” alisema.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.