Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba imetinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa hapo jana baada ya kutoa sare ya 1-1 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.
Mchezo huo ulipigwa majira ya saa 10:00 jioni katika dimba la Chamazi Complex huku Mnyama akitokea nyuma na kusawazisha bao hilo kwa Power Dynamos kujifunga baada ya kushambuliwa sana.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Mnyama ameingia hatua hii kwa faida ya goli la ugenini kwani kwenye mchezo wa kwanza alitoa sare ya 2-2 akiwa ugenini huku mabao hayo yote yakitupiwa kimyani na Cloutus Chama.
Licha ya vijana wa Robertinho kutinga hatua hiyo lakini bado mashabiki wanapata wasiwasi na timu yao kwa namna ambavyo inacheza kwani inakuwa ngumu kuona hata goli litafungwa muda gani.
Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.
Hii inakuwa ni mara ya 6 kwa Simba kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na mara nyingi amekuwa akiishia Robo Fainali. Je msimu huu Mnyama atafika hatua gani kwa kiwango chake?