Yanga Yatua Dar es salaam na Kupokelewa na Mashabiki Zao

Klabu ya Yanga imetua jijini Dar es salaam kutoka Algeria ambapo walikuwa wakicheza mchezo wao wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya USM Alger.

 

Yanga Yatua Dar es salaam na Kupokelewa na Mashabiki Zao

Na mchezo huo ulimalizika kwa Yanga kuhsinda lakini hawakuweza kuchukua Ubingwa huo kutokana na goli la ugenini ambalo USM Alger alipata kama faida kwenye mchezo wa kwanza ambao walicheza wakiwa hapa nyumbani.

Kwenye mchezo wa kwanza, Wananchi chini ya kocha mkuu Nabi walipoteza kwa mabao 2-1 huku faida akiwa nayo mgeni kwani bado Afrika goli la ugenini linahesabiwa tofauti na Ulaya.

Mechi ya pili wananchi walipambana kutafuta mabao mawili pekee ambayo yangeweza kuwapatia taji hilo na kuweka historia hapa Tanzania lakini haikuwa rahisi na kuishia kupata bao moja pekee kupitia Djuma Shaban kwa mkwaju wa penati dakika ya 07.

Yanga Yatua Dar es salaam na Kupokelewa na Mashabiki Zao

Baada ya kuwa washindi wa pili, wamerejea Tanzania na kupokelewa na mashabiki zao huku wakiwapongeza kwa hatua waliyofikia na kuweza kulipa Taifa heshima ya hali ya juu sana.

 

 

Acha ujumbe