Ureno na Norway Wafuzu Safari ya Kombe la Dunia 2026

Mabingwa wa Euro 2016, Ureno, wametuma ujumbe mzito kwa wapinzani wao baada ya kuichapa Armenia 9–1 na kutinga Kombe la Dunia 2026 kwa kishindo. Wakati huo huo, Norway imeandika historia baada ya kufuzu kwa mara ya kwanza tangu 1998, ikiichapia Italia nyumbani kwao kwa ushindi wa mabao 4–1 katika uwanja wa San Siro.

Baada ya matokeo yasiyotabirika dhidi ya Hungary na kisha kipigo cha kushtusha kutoka Ireland, Ureno walihitaji ushindi wa uhakika na wakautoa kwa kiwango cha juu kabisa. Bila Cristiano Ronaldo aliyeapata kadi nyekundu mchezo uliopita, Bruno Fernandes na João Neves walibeba jukumu la ufungaji, kila mmoja akifunga hat-trick mbele ya mashabiki wa Porto.

Ureno na Norway Wafuzu Safari ya Kombe la Dunia 2026

Renato Veiga, Gonçalo Ramos na Francisco Conceição nao waliongeza ladha ya ushindi huo mnono.

Kwa mara ya saba mfululizo, Ureno wanajihakikishia nafasi kwenye fainali za Kombe la Dunia. lakini bado wakisubiri ndoto yao ya kulitwaa kwa mara ya kwanza.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Ireland Yaandika Hadithi Yake, Yaingia Playoffs kwa Dakika ya 96

Ureno na Norway Wafuzu Safari ya Kombe la Dunia 2026

Katika mchezo mwingine wa kuvutia, Troy Parrott aliingia kwenye vitabu vya historia vya Ireland kwa kufunga hat-trick ya dakika za majeruhi iliyowapeleka moja kwa moja kwenye hatua ya mchujo. Bao lake la mwisho, dakika ya 96, lilimgeuza shujaa wa taifa baada ya Ireland kutoka nyuma kwa mabao mawili dhidi ya Hungary.

Parrott, aliyeiumiza Ureno siku chache zilizopita, aliendeleza moto huo na kuwapa Ireland matumaini mapya kuelekea Machi.

Norway Yarejea Kwenye Ramani ya Dunia Baada ya Miaka 28

Ureno na Norway Wafuzu Safari ya Kombe la Dunia 2026

Katika kundi lingine, Italia walihitaji muujiza ili kuwazidi Norway kwa tofauti ya mabao. Walipata matumaini ya mapema kupitia Pio Esposito, lakini ukuta wa Norway ulikataa kupasuka.

Baada ya mapumziko, Antonio Nusa alisawazisha kabla ya Erling Haaland kufunga mabao mawili ndani ya dakika moja. Jorgen Strand Larsen akaongeza la nne na kuzima kabisa ndoto za Italia.

Kwa ushindi huo, Norway imefuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1998 na kwa mtindo.

Italia sasa wanaingia kwenye mchujo, wakimaliza nafasi ya pili.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.