Yanga Kuwavaa Waarabu, Safari Ya Algeria Yaanza Leo

Kikosi cha Yanga SC chini ya Kocha Mkuu Pedro kinatarajiwa kuanza safari mapema leo Novemba 24, 2025 kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la klabu bingwa barani Afrika.

Safari hii ya mapema inalenga kuwapa wachezaji muda wa kutosha kufanya maandalizi kamili, kuzoea mazingira ya ugenini na kujiandaa kikamilifu kwa mtanange unaowakabili dhidi ya JS Kabylie mnamo Novemba 28, 2025.

Yanga Kuwavaa Waarabu, Safari Ya Algeria Yaanza Leo

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS FAR Rabat kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Yanga SC inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na morali ya juu. Bao pekee kwenye mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji Prince Dube aliyemalizia kwa ustadi pasi safi ya kiungo Mudathir Yahya.

Winga huyo kutoka Zimbabwe amekuwa mhimili muhimu kwenye safu ya ushambuliaji, na mashabiki wa Yanga wanategemea moto huo kuendelea katika safari ya Algeria.

Yanga SC inakutana na JS Kabylie ambayo inakuja kwenye mchezo huo ikiwa na majeraha ya kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa vinara wa Kundi A, Al Ahly ya Misri. Pamoja na matokeo hayo mabaya, Kabylie wanatarajiwa kuwa hatari zaidi wakiwa nyumbani mbele ya mashabiki wao.

Yanga Kuwavaa Waarabu, Safari Ya Algeria Yaanza Leo

Kocha Pedro anaelezwa kutaka kikosi chake kiwasili mapema ili kufanya mazoezi kwa siku kadhaa, kuifahamu hali ya hewa, uwanja na mazingira ya mji watakaocheza, jambo ambalo linaweza kuamua uimara wao uwanjani.

Malengo ya Yanga kwenye safari hii ni moja tu, kuondoka Algeria na alama. Iwe moja au tatu, mabingwa hao wa Tanzania Bara wanataka kuiweka Kundi B mikononi mwao mapema kabla ya mechi za marudiano. Mashabiki wa Wananchi nchini kote wanakitakia kikosi chao safari njema wakiamini kuwa morali ya ushindi dhidi ya AS FAR inaweza kugeuka kuwa nguvu ya kupata matokeo muhimu ugenini.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.