Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ana imani Thomas Partey atasalia Emirates, licha ya kuwasili kwa nyota wa Uingereza Declan Rice.
Kiungo huyo wa kati wa Ghana amekuwa akihusishwa na kuhamia Al-Ahli ya Saudi Arabia, lakini Arteta alisema bado ni sehemu muhimu ya mipango yake.
Arteta alisema: “Bila shaka, Thomas Partey ni mchezaji muhimu sana kwetu na kwangu. Nataka awe kwenye timu. Kila nilipozungumza naye na kila ninapokuwa na mazungumzo naye mapenzi yake ni kukaa nasi. Kwangu mimi, hakuna kitu huko kabisa.”
Alisema kuwasili kwa Rice haimaanishi kupunguzwa kwa jukumu la Partey kwani wanaweza kucheza pamoja na hiyo ilikuwa katika mipango yake kwani wanataka kuboresha kikosi na kuwa na ubora zaidi.
Tunahitaji wachezaji ambao wanaweza kucheza pamoja lakini tunahitaji wachezaji walio katika nafasi sawa ambao wanaweza kupigania nafasi zao. Ni kitu ambacho hatujapata kwa miaka michache iliyopita na tulitaka kuboresha hilo na ndiyo sababu tulinunua Declan. Alisema kocha huyo.
Arsenal walimaliza nafasi ya pili nyuma ya Manchester City katika Ligi kuu msimu uliopita, wakiwa wameongoza msimamo kwa muda mwingi wa kampeni uzoefu ambao Arteta anaamini utawasaidia wachezaji wake wanapotazamia kupiga hatua inayofuata.
Kocha huyo anadhani kilichotokea mwaka jana labda kilikuwa muhimu ili kujifunza masomo wanayopaswa kujifunza ili kuwa bora na kufanikiwa zaidi na kufikia kile wanachotaka kufikia.
Kiwango kinaenda kupanda. Timu zinazidi kuwa bora na ligi inazidi kuimarika, itazidi kuwa ngumu. Lazima wawe bora zaidi. Wanapaswa kucheza vizuri zaidi na wanapaswa kufanya mambo vizuri zaidi kuliko walivyofanya mwaka jana. Hilo ndilo wanalofanyia kazi kwa sasa.
Olexsandr Zinchenko, ambaye alivutia sana katika msimu wake wa kwanza baada ya kuhama kutoka Manchester City, anaamini wanaweza kupiga hatua hiyo.
Alisema: “Nilisema mara nyingi huko nyuma, nina hisia na, harufu ambayo ningesema, kwamba wakati wa Arsenal unakuja. Kwa bahati mbaya msimu uliopita hatukufanikiwa kile tulichotaka lakini ilikuwa masomo mengi mazuri kwetu wakati wa msimu na, kwa hakika, itatusaidia wakati ujao. Nimejawa na imani kwa hivyo tuone kitakachotokea.”
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine amelazimika kukabiliana na mambo mengi nje ya uwanja baada ya uvamizi wa Urusi nchini mwake na kuwataka watu kuendelea kuunga mkono pambano lao.
Alisema: “Ninajua baadhi ya watu wamepata uchovu kutokana na vita hivi lakini hatuwezi kukata tamaa. Sote tunahitaji kupigania uhuru wetu, uhuru wetu. Leo ni Ukraine, kesho inaweza kuwa nchi yako. Ndio maana tunahitaji kushikamana na kupigana hadi mwisho.