Klabu ya Dodoma Jiji imechakazwa jana kwa mabao 4-1 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho la Azam katika Dimba la Chamazi.

Mchezo huo ulishudiwa kwa mabao mengi toka timu hizo kukutana huku Dodoma wakitoka kupoteza mchezo wao uliopita wa Ligi, halikadhalika kwa vijana wa Kally Ongala nao wametoka kupoteza mchezo wao.
Walima zabibu baada ya kuwa wametanguliwa mabao mawili kwa moja kwenye kipindi cha kwanza, walipata penalti lakini mchezaji ambaye wamemsajili Stephen Sey akapaisha mkwaju huo.m

Hivyo mpaka sasa vijana Chamazi wao ni wababe wanapokutana na Walima Zabibu kwani mechi sita walizokutana wameshinda tano na kutoa sare mchezo mmoja kati yao hadi sasa.

