KMC Atatoboa Leo Mbele ya Singida Big Stars?

Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara inaendelea kwa michezo miwili ambapo mechi ya mapema saa 10:00 jioni itakuwa ni kati ya KMC dhidi ya Singida Big Stars.

 

KMC Atatoboa Leo Mbele ya Singida Big Stars?

Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa majira ya saa 10:00 jioni huku wenyeji wa mchezo KMC wakiwa na hali mbaya wakishikilia nafasi ya 14 akiwa nafasi mbili kutoka mkiani kwenye msimamo wa ligi.

Ushindi wa leo wa Kino Boys utawafanya wapande hadi nafasi ya 12 kwenye ligi. Je wataweza kuifunga Singida Big Stars ambao wapo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi na wanahitaji kushiriki Kombe la Shirikisho msimu ujao?

KMC kwenye mechi zake 27 alizocheza ameshinda mechi sita, sare nane na wamepoteza michezo 13 hadi sasa akiwa na pointi 26 kwenye msimamo huku akiwa amepoteza mechi mbili mfululizo kwenye ligi.

KMC Atatoboa Leo Mbele ya Singida Big Stars?

Wakati Singida Big Stars wao wapo nafasi ya nne, wakiwa wameshinda mechi 15, sare sita na wamepoteza michezo sita hadi sasa. Wamekusanya pointi zao 51 na wamepoteza mchezo uliopita.

Mara ya mwisho kukutana WanaKino Boys walipoteza kwa bao 1-0 katika dimba la Liti Singida. Leo watalipiza kisasi?

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.