RAGE AKUBALI MZIKI WA PACOME

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Ismael Aden Rage, ameweka wazi kuwa anakoshwa na ubora wa kiungo wa Yanga Pacome Zouzoua na kudai kuwa kovh wa Ivory Coast anapaswa kuwa na majibu mazito, kwanini alimuacha nyota huyo. 

RAGE AKUBALI MZIKI WA PACOME

Rage amesema, anatamani kumuuliza Kocha wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast kwanini hakumuita Pacome kwenye Afcon, lakini anashindwa Kwa kuwa Hana namna ya kumpigia.

“Ningekuwa na namba ya kocha wa timu ya Ivory Coast basi ningemwambia wanamuacha vipi kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast”

Pacome ZouZoua ni mchezaji mzuri sana anastahili kucheza timu ya Taifa kocha inakuaje anawaamini wachezaji wa Europe akati una mtu kama Pacome yupo kwenye kiwango bora. Alimaliza hivyo.

Acha ujumbe