KIUNGO mshambuliaji fundi wa Yanga, Pacome Zouzoua amesema kuwa wamejifunza wamejifunza baada ya kipigo kutoka Ihefu FC, lakini watarudi wakiwa katika kiwango bora kuelekea michezo inayofuatia.
Yanga juzi ilikutana na kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Ihefu FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Higland Estates, Mbarali Mkoani Mbeya.
Katika mchezo huo, Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Pacome huku ya Ihefu yakipachikwa na Lenny Kissu, Charles Ilanfya.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika Pacome alisema kuwa kipigo hicho ni somo kwao wachezaji, hivyo watarejea imara katika michezo inayofutia.
Pacome alisema kuwa kocha wao Muargentina Miguel Gamondi wameona upungufu uliosababisha wapoteze mchezo huo huku akiamini atafanyia maboresho ili mchezo wao wapate ushindi.
“Katika soka kufungwa ni lazima, ngumu timu kupata ushindi katika kila mchezo, na bila kufungwa mpira wa miguu usingekuwa na mvuto.

