Azam FC waliambulia pointi moja ugenini kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa jana Jumapili ikiwa ni mzunguko wa pili.
Mashabiki ndani ya Uwanja wa Sokoine walishuhudia Matokeo yakiwa Tanzania Prisons 1-1 Azam FC. Ni Samson Mbangula alianza kupachika bao mapema dakika ya 5 likawekwa usawa na Fei Toto dakika ya 54 kwa mkwaju wa penalti.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Kiungo Fei Toto alifunga na anafikisha mabao 9 ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ni mfungaji namba moja kwa wazawa huku akiwa ni namba mbili kiujumla kwa kuwa kinara ni Aziz KI wa Yanga mwenye mabao 10.
Kwa upande wa Tabora United nao walikomba pointi moja dhidi ya Singida Fountain Gate, mapema Singida Fountain Gate walipata bao kupitia kwa mshuti wa Yahya Mbegu akiwa nje ya 18, ilikuwa dakika ya 51, mwamba John Nakibinge akapachika bao akiwa ndani ya 18 kwa utulivu na header dakika ya 83.